Wednesday, September 6, 2017

Tangazo kwa watumishi wenye madai ya mapunjo ya mishahara

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI NANYAMBA, ANAWATANGAZIA WATUMISHI WALIOPO KATIKA HALMASHAURI YA MJI NANYAMBA (WALIOPO KWENYE ORODHA HII NA WASIOKUWEPO) WENYE MADAI YA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA WANAOLIPWA MISHAHARA KUPITIA ORODHA YA MALIPO YA SERIKALI (PAYROLL), KUFIKA KATIKA OFISI YA MKURUGENZI WA MJI, KUANZIA TAREHE 06 HADI 09 SEPTEMBA 2017, PIA TAREHE 11 HADI 14 SEPTEMBA 2017 KWA AJILI YA KUJAZA FOMU ZA MAPUNJO YA MISHAHARA (Salary Arrears claim form). HII NI KUTOKANA NA TAARIFA ZAO ZA MADAI KUPATA HITILAFU KATIKA MFUMO WA TAARIFA ZA KIUTUMISHI NA MISHAHARA(LAWSON)

WATUMISHI HAO WENYE MADAI WANATAKIWA KUWA NA NAKALA ZA NYARAKA ZIFUATAZO;

WENYE MADAI YA MISHAHARA KUTOKANA NA KUPANDISHWA VYEO/MADARAJA(promotion)

  • Nakala ya barua mpya ya kupandishwa cheo/daraja (promotion)
  • Nakala ya barua ya zamani ya kupandishwa cheo
  • Nakala ya hati ya mshahara (salary slip) kabla ya mabadiliko ya mshahara
  • Nakala ya hati ya mshahara baada ya mabadiliko ya mshahara.

WENYE MADAI YA MISHAHARA KUTOKANA NA AJIRA MPYA

  • Nakala ya barua ya ajira
  • Nakala ya barua ya kupangiwa kituo cha kazi
  • Nakala ya hati ya mshahara (salary slip) ya mshahara wa kwanza.

MUHUMU 

Kila mtumishi awasiliane na Mkuu wa Idara  kabla ya kuonana na Ofisi ya Utumishi.
 Tangazo hili limetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba

Bofya hapa chini kuona Jina lako.

No comments:

Post a Comment

Tangazo kwa watumishi wenye madai ya mapunjo ya mishahara

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI NANYAMBA, ANAWATANGAZIA WATUMISHI WALIOPO KATIKA HALMASHAURI YA MJI NANYAMBA ( WALIOPO KWENYE ORODHA HII N...